23 Desemba 2023 - 15:33
HAMAS: Azimio la Baraza la Usalama la UN kuhusu Gaza halitoshi kukidhi mahitaji

Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imetoa mjibizo kwa azimio lililopitishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Ukanda wa Gaza na kusisitiza kuwa halitoshi na halikidhi mahitaji.

Kwa mujibu wa IRNA, harakati ya Hamas imesisitiza kuwa kupitishwa kwa azimio hilo hakulingani na mahitaji na matakwa ya hali mbaya ya maafa yanayoshuhudiwa hivi sasa katika Ukanda wa Gaza. Harakati hiyo imeongeza kuwa serikali ya Marekani imewasilisha azimio hili kwa namna ambayo inatoa ruhusa kwa wavamizi wa Kizayuni kuendeleza mauaji na uharibifu.Hamas imesema Baraza la Usalama linapaswa kuulazimisha utawala ghasibu wa Kizayuni uruhusu misaada ya kutosha iingizwe kwenye Ukanda wote wa Gaza hususan maeneo ya kaskazini.

 Hatimaye, na kufuatia mashinikizo ya kimataifa kwa Marekani -ambayo ni muungaji mkono mkuu wa utawala ghasibu wa Israel- ya kutaka utawala huo katili usitishe mashambulio yake ya kinyama dhidi ya Gaza unayoyafanya kwa lengo la kulipiza kisasi kwa operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa usiku wa kuamkia leo lilipitisha azimio la kutaka kuongezwa zaidi misaada wa kibinadamu kwa ajili ya Gaza, baada ya upigaji kura wa kupitisha azimio hilo kucheleweshwa kwa wiki nzima kutokana na ukwamishaji wa Marekani.../


342/